Dr. Luis Shika Kid Tajiri anaye itikisa Tanzania

Sehemu ya 1

Dr Shika amesimulia historia yake na kubainisha mambo kadhaa kuhusu Maisha yake
1.Taaluma yake
Dr Luis Shika Kid ni daktari wa binadamu, historia yake inamuonesha kuwa alienda urusi mwaka 1984 kwaajiri ya kusomea udaktari ambapo alisoma degree ya kwanza Md (Doctor of Medicine) na kumaliza 1991 ilimgharimu miaka7, Mwaka huo huo aliunga Degree ya pili Msc in Infectious diseases na kumaliza mwaka 1993. Degree ya 3 (PhD) alihama kutoka kusini mwa urusi mpaka Moscow ambako aliendelea degree yake (Phd) baada ya hapo akaingia degree ya 4 Doctor of medical science ambayo ni degree inayo mfanya na yeye atambulike kuwa pia ni msomi kulingana na viwango vya kimataifa.
2.Shughuli zake baada ya kumaliza masoma
Dr Shika anaeleza kuwa baada ya masomo alibaki nchini Urusi akifundisha madakari chuo fulani huko urusi. Baada ya muda kidogo tarehe 28/07/1999 alifungua kampuni inayoitwa Lancefort inayo jihusisha na utengenezaji pamoja na usafirishaji wa kemikali za viwandani na kwa kiasi kikubwa kemikali za kilimo (mbolea nk.). Alikuwa akipata order kubwa toka kampuni mbalimbali duniani japokuwa hakupata order nyingi toka Tanzania.
Aliwezaje kumiliki kampuni kubwa hivo, pesa alizitoa wapi?
Dr Luis Shika Kid anaelezakuwa alipo kuwa akifundisha madaktari huko Urusi aliweza kupata pesa kiasi ambazo alizitumia kufungua kampuni yake na kununua maghofu ya viwanda vilivyo kuwepo tangu enzi za communism na kufa baada urusi kuporoka kiuchumi,Dr anaeleza kuwa aliweza kununua kiwanda kimoja baada ya kingine. Safari ya mafanikio ikawa imepamba moto ambapo viwanda vilifika zaidi ya 10.
Nini Msitakabari wa kampuni hiyo kwa sasa, je inaendelea kufanya kazi?
Dr. Shika anaeleza kuwa kampuni yiyo bado ipo kazini hadi leo hii, na anakili kuwa kuwepo kwake Tanzania kwa muda mrefu hakuathiri shughuli za kiutendaji za kampuni hiyo, kwani kampuni imeundiwa misingi bora ya kiuongozi kuanzia Director General mpaka mfagiaji. Pia Raisi wa kwanza na wa mwisho wa shirikisho la Kisoviet Mikhail Sergeyevich Gorbachev ni mwenyekiti wa bodi of directorate ambaye ni mshauri mzuri sana na anachangia uimara wa kampuni hiyo.

Comments

Popular Posts